emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa

Jisajili, Tukutambue, Tukutambulishe


NIDA WAPEWA ELIMU YA MAGONJWA SUGU YASIYOAMBUKIZA

IDA WAPEWA ELIMU YA MAGONJWA SUGU YASIYOAMBUKIZA

Na. Musa Kadiko

Kundi kubwa la watumishi wa umma, lipo katika hatari ya kupata magonjwa sugu yasiyoambukiza kutokana na mtindo wa maisha ikiwa ni pamoja na  tabia ya kutofanya mazoezi na ulaji usiozingatia lishe bora.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, George Seni wakati akifungua mafunzo kwa watumishi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) wa mikoa ya Katavi, Kigoma na Rukwa, kuhusu VVU, UKIMWI na magonjwa sugu yasiyoambukiza, Oktoba 04, 2025 Mpanda Mkoani Katavi.

George Seni, amesema kuwa, watumishi wa umma wapo katika hatari kubwa ya kupata magonjwa yasiyoambukiza ukiwemo ugonjwa wa shinikizo la damu na sukari, hivyo amewaasa watumishi kufanya mazoezi mara kwa mara pamoja na kuzingatia ulaji wa vyakula bora.

Katika mapambano dhidi ya UKIMWI na magonjwa sugu yasiyoambukiza, Mkurugenzi wa Fedha na Utawala amesema kuwa, NIDA itaendelea kutoa elimu kwa watumishi kupitia programu mbalimbali pamoja na kuwawezesha kushiriki katika michezo ili kuimarisha afya ya akili na mwili.

Kwa upande wake Afisa Muuguzi kutoka Hospitali ya Wilaya ya Mpanda Enderson Fidel amewasisitiza watumishi wa NIDA kulinda afya zao dhidi ya VVU na UKIMWI kwa kujiepusha na ngono zembe, kutumia kinga pamoja na kuwa na utaratibu wa kupima afya zao mara kwa mara na kupata ushauri wa kitaalamu “UKIMWI upo na sote tunapaswa kuchukua tahadhari ya kujilinda na ugonjwa huu, kwa kuacha ngono zembe, tutumie kinga na kujenga utaratibu wa kupima afya zetu sambamba na kufata ushauri wa daktari” alisisitiza Afisa Muuguzi huyo.

UCHAGUZI MKUU OKTOBA 29, 2025

Kura Yako Haki Yako Jitokeze Kupiga Kura