
NIDA) yakabidhiwa Cheti cha Utoaji wa Huduma Bora kwa Wananchi
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imekabidhiwa Cheti cha Utoaji wa Huduma Bora kwa Wananchi kutoka kwa Kampuni ya TAKADIR COMPANY LIMITED.
Hafla ya makabidhiano imefanyika katika Ofisi za NIDA Zanzibar tarehe 03 Oktoba 2025, ambapo cheti hicho kimekabidhiwa kwa Mkurugenzi wa Ofisi ya Uratibu NIDA Zanzibar, Bw. Abdallah M. Omar.
Akizungumza baada ya kupokea cheti hicho, Bw. Abdallah ameishukuru kampuni ya TAKADIR COMPANY LIMITED kwa kutambua jitihada za watendaji wa Mamlaka katika kutoa huduma bora kwa jamii. Amesema kutambuliwa huko kutachochea hamasa ya utendaji na kuongeza ari ya kujitoa zaidi katika kutekeleza majukumu yao, sambamba na kuiweka NIDA katika nafasi ya kuwa mfano wa kuigwa kwa taasisi nyingine.